...hii ni mtaa hadi mtaa...

Saturday, May 18, 2013

INAVYOSEMEKANA MADEE KACOPY NA KUPASTE WIMBO WAKE WA "POMBE YANGU" KUTOKA KWA HUYU JAMAA! JIOONEE MWENYEWE HAPA

Je ni kweli kua Madee kacopy na kupaste! Ukisikiliza vizuri wimbo wa madee na huu hapa chini katika video utagundua kama zinaendana hivi kwa kiasi kikubwa.
HII NDIO NYIMBO YA AMA THE MAKER-"ULE MSOGA"


COMPARE NA VIDEO HII MPYA YA MADEE

comments

MTOTO ALIYEPIGWA MAPANGA NA BABA YAKE AFARIKI DUNIA


Mtoto Devotha Gerald (4) aliyepigwa mapanga na baba yake, polisi mstaafu Samson Bwire Amefariki dunia baada ya jitihada za madaktari kuokoa maisha yake kushindikana...
 
Mtuhumiwa wa tendo hilo ambaye naye alipigwa vibaya na wananchi wenye hasira yuko mikononi mwa jeshi la polisi....
 
Tendo hili lilitokea mkoani Shinyanga. 
Kama haukuona habari hiyo ya kusikitisha, ya kushambuliwa mtoto huyo, iliyotokea juzi usiku, nenda kwenye link ifuatayo: Polisi mstaafu amcharanga mapanga mwanae wa miaka 4

comments

KESI YA MTOTO ANAYETUHUMIWA KUMUUA MTOTO MWENZIE KWA KUMKATA KICHWA "RAMA MLA WATU" YAZUA MAKUBWA MAHAKAMAN

MAMA wa marehemu Salome Yohana, Pendo Dustan Mushi (picha ndogo katikati) ambaye kichwa cha mwanaye huyo kinadaiwa kukutwa na Ramadhan Suleiman ‘Rama mla watu’ amezua timbwili Mahakama Kuu, jijini Dar akitaka kujua hatma ya kesi hiyo ya mauaji.Tukio hilo lilitokea Mei 16, mwaka huu ambapo mama huyo alinaswa na kamera yetu akilalamika huku akilia kwa uchungu akitaka kujua hatma ya kesi hiyo ya mwanaye ambayo imedumu tangu mwaka 2008.
“Nataka kujua hatma ya kesi ya mauaji ya mwanangu, mara kwa mara nimekuwa nikija hapa mahakamani na kurudi bila kujua chochote kinachoendelea.
“Inaniuma sana kuona hukumu haitolewi, licha ya mwanangu kupoteza uhai muda mrefu lakini siwezi kumsahau, nimekuwa nikilia kila nikikumbuka kifo chake na hasa siku za kesi ndiyo huwa naumia sana,” alilalamika mama huyo na kuongeza:
“Hata mwenendo mzima wa kesi siufahamu, nilisikia kwenye vyombo vya habari kuwa kesi yake inasomwa leo lakini mpaka dakika hii sielewi chochote.”

Baada ya kulalamika sana, mama huyo alipata msaada wa kufikishwa kwa makarani wa kesi za jinai mahakamani hapo ambao walimhakikishia kuwa kuwa kesi hiyo itatajwa Mei 24, mwaka huu mbele ya Jaji John Temba wa mahakama hiyo.
Rama ambaye alijizolea umaarufu mkubwa mwaka 2008 baada ya kukamatwa akiwa na kichwa cha mtu kinachodaiwa kuwa ni cha Salome, hadi sasa anasota Gereza la Segerea Jijini Dar akisubiri mwenendo wa kesi hiyo.

comments

KANYE WEST NI "SHOGA" NA ANA BWANA PARIS-"MPENZI WAKE KIM KARDASHIAN AFUNGUKA"

Jarida la In Touch limeandika, muigizaji nyota ambaye kwa sasa ni mjamzito Kim Kardashian, anahofia boyfriend wake Kanye West huenda akawa ni shoga na ana boyfriend jijini Paris.

Kwa mujibu wa jarida hilo, Kardashian anapata wasi huo sababu watangazaji wengi wa kwenye mitandao wanamuhisi kwamba boyfriend wake huenda akawa yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanaume ambaye aliwahi kumtengenezea nguo aitwaye Riccardo Tisci.”

Japo yeye anamuita "rafiki" alilieleza kwenye jarida hilo, “Kim alifunguka zaidi na kusema. Kama kweli ikitokea kwamba Kanye yupo na Riccardo kimapenzi, itamumiza sana - zaidi ya nilivyowahi kuumizwa kwenye maisha yake yote.”
Jarida la In Touch limeandika, “Kuna vielelezo ambavyo Kim hawezi kuvipinga,” huku vikiorodheshwa, “Katika kipindi chote ambacho Kim ni mjamzito Kanye amekuwa akitumia muda wake mwingi akiwa karibu na Riccardo kwenye jiji hilo lililopo nchini Ufaransa… Na hivi karibuni Riccardo amenunua nyumba New York umbali wa nusu ya maili toka sehemu ambayo Kanye anaishi.”
comments

KAULI YA CHID BEENZ BAADA YA KUCHEZEA KICHAPO KUTOKA KWA KALAPINA MAISHA CLUB

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Chid Beenz, amesema watu wengi wanayafatilia maisha yake sababu yeye ni msanii mkubwa na ni star zaidi yao.

Chid ambaye masikani yake ni Ilala Flats jijini Dar, amesema kitendo cha watu kuwa wanamfatilia kwa yale au kile anachokifanya sababu yeye ni msanii mkubwa na wasanii wengine inabidi  wamfuatilie.
Maoneno hayo yalikuja baada ya kumuuliza swali juu ya alichokisema Kala Pina, kwamba Chid ameathiriwa na madawa, ndipo Chid alipojibu, “Sasa yeye mwenyewe mbona anavuta ganja, vitu kibao anafanya, sasa kwani mbona mimi simtangazii kwenye media,  mimi sina habari, yeye kama ananifatilia hivyo nashukuru  kumbe mimi ni bonge la star.
KUANGALIA VIDEO YA CHID BEENZ AKICHEZEA KICHAPO 
Aliendelea Chid akisema, “Umeona mwandishi watu wanahisi nimepotea, wakati kina Pina wananifatilia hadi maisha yangu, oohhh navuta nini…., sijui nimetoboa nini….., nilihisi hajawahi kuniona na kaona nimefanya nini…., nimevaa niko nini……, kumbe wananiona hivyo hadi nafanya nini, safi sana…” Alimalizia Chid Beenz…

comments

DADA WA DIAMOND "ESMA" AZUNGUMZIA JUU YA HARUSI YA DIAMOND NA PENNY

http://3.bp.blogspot.com/-7_ZNw9Oygj4/UYTcJhFaLZI/AAAAAAAAGJs/VSim5EztCmI/s1600/diamond.jpg
Esma Abdul ambae ni dada yake mwimbaji staa wa Tanzania, Diamond Platnums, amesema wamejiandaa vizuri kwa ajili ya harusi ya Diamond ambae anatarajiwa kumuoa mtangazaji wa TV aitwae Penny.

Esma ambae anaishi nyumba moja na kaka yake amesema, "Tumemkubali sana wifi yetu na tunampenda kwa sababu mtu yeyote mimi nitakaetambulishwa siwezi nikamkataa, manake nikimuingilia kwenye mapenzi yake na yeye ataniingilia kwenye mapenzi yangu."




Huu ni mwezi wa tano toka Esma amjue wifi yake ambae ni Penny, anasema nyumbani amekubalika na mipango ya harusi inaandaliwa japo hajui ni lini itafanyika, manake hiyo ni siri kwa sasa.


Zaidi ya wiki tano zilizopita, Diamond aliongea na kusema ndoa yake imekaribia kufungwa na huyo mkewe mtarajiwa ambae ni mjamzito lakini pia akathibitisha kumnunulia gari la kutembelea aliloliagiza nchini Japan - Hyundai IX 35.

Mpaka sasa Mwimbaji Diamond Platnums ambae aliongoza kwa kuwa msanii wa Tanzania alieandikwa sana kwenye internet 2012, ameshaingia kwenye headlines za kuwa mapenzini na mastaa wa kike Tanzania kipindi cha nyuma kama Jokate, Wema Sepetu na wengine. 

comments

Friday, May 17, 2013

WASICHANA WA CBE,UDSM NA VETA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUJIUZA-"HAYA NDIO MAJINA YAO NA VYUO WANAVYO SOMA"

Wanafunzi wa kike wa chuo kikuu cha Dar es salaam [UDSM],Chuo cha elimu ya biashara [CBE]na chuo cha mamlaka ya Elimu na ufundi  stadi [VETA],Dar es salaam ,wamefikishwa katika mahakama ya jiji samora wakidaiwa kufanya biashara ya kuuza mili yao.
Washitakiwa hao waliokamatwa  katika eneo la kona Baa Ambiance Sinza wilayani kinondoni ambao ni miongoni mwa wanawake 35 wanaodaiwa kufanya biashara hiyo na wote walifikishwa mahakamani hapo.
Kesi hiyo ilikuwa chini ya hakimu Willian Mtaki ambapo muendesha mashitaka,bwana John Kijumbe,alisema wasichana hao walikamatwa katika mazingira tofautitofauti.
Wanafunzi hao ni Yasinta Kilimo mwenye miaka 21 CBE mkazi wa upanga,Morin Masatu miaka 19 UDSM,mkazi wa kinondoni na mwanafunzi wa VETA aliyefahamika kwa jina moja la Khadija.
“Nilikwenda pale baa kuchukua simu yangu ambayo ilipotea hivyo waliniita nikaichukue ndipo askari wa jiji wakanikamata,”Alisema Khadija akijitetea.
Kwa mujibu wa bw. Kijumbe washitakiwa  hao wamekosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili au kulipa faini ya kulipa sh. 200,000.
Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa tena mei 28 mwaka huu,ambapo washitakiwa wote walipelekwa Segerea
Wakati huohuo, jeshi la Polisi mkoa wa kinondoni , limewakamata watuhumiwa 716 waliokuwa wakijihusisha na biashara ya kuuza miili kati yao wanaume 38 na wanawake 678.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela, alisema watu hao walikamatwa kwenye msako uliodumu kwa miezi sita kwenye maeneo mbalimbali ya Kinondoni.

Maeneo hayo ni baa, kumbi za starehe, madanguro, sehemu za wazi katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, na makaburini ambapo kati ya wanaume waliokamatwa wengine ni mashoga pamoja na wateja wa machagudoa.
“Msako huo ulifanyika Maisha   Club, Coco Beach, Barabara ya Tunisia , Travertine Hotel, Tandale Uwanja wa Fisi, Ambiance Club, Shekilango pamoja na Mwinanyamala” Alisema
Kamanda Kenyela aliongeza kuwa , jeshi hilo pia limewakamata raia 12 kutoka nchini Ethiopia walioingia nchini bila kibali kati ya Mei 2 na 6, mwaka huu katika eneo la Kimara Mwisho na Tegeta Kibaoni.
Alisema kukamatwa kwao kulitokana na taarifa walizozipata kutoka kwa raia wema waliowaona maeneo.

comments

HIZI NDIZO PICHA ZA NUSU UCHI ZA KUNDI LA "ZE KOMEDI' ZILIZOVUJA

Picha za aibu  zinazowaonesha wasanii wa kundi la Ze Komedi wakiwa kwenye fukwe moja ya huko Kigamboni zimezua balaa kubwa ......
 Happy  kabla  hajavua  nguo.... 
==
Mtandao  huu  umefanikiwa  kuzipata  picha  hizi  kutoka  kwa  msomaji  wetu  mpendwa  ambaye  kwa  uzalendo  wake  ametutumia  kwa  njia  ya  email  huku  akielezea  kwa  kifupi  kuhusu  sakata  hilo  la  aibu.....
 
Happy akichezewa matiti na master Face huku akichekelea
Huyu  ni  Happy na Master  Face  wakifanya  Uchafu wao....Hapa  wanatomasana  kabla ya uzalendo kuwashinda  na  kuamua  kuvunja  amri  ya  sita...
Vipi  baby....umezidiwa.....!!!! Aibu tupu 
==
Mdau  huyo  anaripoti  kwamba, kundi  hilo  liliingia  ndani  ya  ufukwe  wa  Chadibwa  na  kuanza  kufanya  mambo  ya  aibu  mbele  ya  watu..... 
Wasanii  walioongoza  kwa  mambo  ya  aibu  ni  mdada  mmoja  aliyejulikana  kwa  jina  la HAPPY  ambaye  ni  mrembo  aliyejigeuza  mbwa  na  kukubali  kushikwashikwa  ovyo  matiti  yake  na  viungo  vingine  "sensitive"  bila  kujali  watu.....

 Matiti  bado  yanaendelea  kuteswa
Kiwewe  naye  alikuwa  kivyake  na  wakwake.....
  Mbali  na  Happy, kulikuwa  na Msanii KIWEWE ambaye  yeye  alikuwa  akijimilikisha  VIUNO  vya mabinti  hao  bila  aibu..... 
 Achilia  mbali Kiwewe, alikuwepo  pia  MANAIKI SANGA  ambaye  naye  alikuwa  akikumbatia  watatu  watatu....Cha  ajabu  ni  kwamba, yeye  alikuwa  kavaaa, akina  dada  walikuwa  uchi.....
 Aliyetia  aibu  ya  mwaka  ni MASTER FACE ambaye  kwa  mujibu  wa  mdau  alitutumia  picha  hizi  ni  kwamba  yeye  na HAPPY  walifikia  hadi  hatua  ya kuvunja  amri  ya  sita  nyuma  ya  gari.....!!!!
Uzalendo uliwashinda wakaamua  wamalizane....
 Asante  sana  mdau  kwa  picha  na  maelezo.....
comments

MLINZI ACHINJWA KAMA KIKATILI DAR

Mlinzi wa baa ya Darajani Stop Over iliyo kando kando ya barabara kuu ya Morogoro Dar es salaam jirani na daraja la Mzambarauni  Bw Mika Athumani amechinjwa na majambazi usiku wa kuamkia leo.


Habari zilizopatikana eneo la tukio zilidai kwamba majambazi hayo yalivamia baa hiyo iliyojitenga usiku wa manane na kumvamia mlinzi huyo na kumchinka kama kuku na baadae kuvunja baa hiyo na kuimba vitu mbali mbali.

                          
Mwili wa marehemu ukiwa ndani ya gari, la polisi kufuatia mwili huo kutenganiswa vibande viwili..

                        


Sehemu aliyochinjiwa mlinzi huyo aliyefahamika kwa jina Mika Athumani.
Akihojiwa na mwandishi wetu,  mmiliki wa baa hiyo Bw Salvatory Mushi alidai kwamba majambazi hao walimvamia mlinzi wake na kumchinja na baadae walivunja Counter ya baa hiyo pamoja na duka ililipojirani na baa hiyo na kuiba vitu mbali mbali.  

Alipoulizwa kwamba kuna taarifa zinadai kwamba mlinzi huyo alikutwa akiwa amelala Bw Mushi alisema"  inawezekana lakini hakuna mtu mwenye uhakika na jambo hilo kwani sote hatukuwepo,wakti tukio hilo linatokea"

                                 
Mwananachi akishuhudia damu ya mlinzi huyo kwa hudhuni
                               
Baskeli ya Mlizni huyo ikiwa imetapakaa damu ambapo inadaiwa mlinzi huyo alikuwa amelala kwenye eneo hilo
                                    
Redio ambayo majambazi hayo waliiangusha nje ya baa hiyo
                                     
                   
Majaira ya saa 12 asubuhi ya leo wananchi walishuhudia maduka mawili ya baa hiyo yakiwa wazi huku mwili wa mlizni huyo umekutwa upande wa baa ukiwa umechinjwa na kutenganishwa kichwa na mwili
                         
              
Umati wa watu ukishuhudia tukio hilo muda mfupi uliopita
                                
                           
                        
Gali la polisi likiondoka eneo la tukio na mwili wa marehemu
                              
  
Wananchi nao waliondoka eneo hilo la tukio
                                 
Mmiliki wa baa hiyo Bw Salvatory Mushi akihojiwa na waandishi wa habari eneo la tukio
                          
Majirani wa eneo hilo wakihojiwa na waandishi wa habari
Baadhi ya watu waliokuwepo eneo hilo la tukio walidai kwamba mlinzi huyo alikuwa amelala hivyo majambazi hayo yalimvamia na kumpora siraha zake na kishi kumchinja shingoni..
Mwandishi wetu alishuhudia mtoto wa marehemu pamoja na mjukuu wa marehemu wakiangua vilio eneo la tuko baada ya kuuona mwili wa mazazi wao aliyeuwawa kikatili baadae wote wawili walipanda gari la polisi na kuondoka nao.
comments

TID AAMBULIA MATUSI KWA WASHABAKI WAKE BAADA YA KUGOMA KUSHIRIKI KWENYE SHOW YA LADY JAY DEE


TID a.k.a MNYAMA  leo amejikuta  akiambulia  matusi  ya  nguoni  baada  ya kuitosa  show  ya  Lady Jaydee  na  kuandika  chenga  zake  katika  Account yake ya Facebook....
                          
Hizi  ni  comment  za  hao mashabiki  wake  walioamua  kumharibia  siku  yake.....



comments

"KANGAMOKO" WAKAMATWA KWA KUJIUZA KINONDONI

JESHI la Polisi Mkoa wa Kinondoni, linalishikilia  baadhi ya wanenguaji wa kundi maarufu kwa  kucheza maungo yakiwa wazi ‘Kanga Moko na Laki si Pesa’, gazeti la Tanzania Daima la leo l ina hatimiliki ya hii habari.Watuhumiwa hao wamekamatwa sambamba  na watu wengi wanaofanya biashara ya kuuza miili yao, kufanya mapenzi hadharani
 na vitendo vya kishoga.Akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es salaam, Kamanda wa Polisi wa   Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema kuwa kundi hilo sambamba na  watu hao walikamatwa katika maeneo ya   Hoteli ya Travertine, Ambiance Club,   Kinondoni Makaburini, “Tumewakamata hao  wanaofanya mchezo maarufu wa  Kangamoko na Laki si Pesa na tayari  wanafikishwa mahakamani muda wowote  na msako bado unaendelea ili kudhibiti vitendo hivyo na michezo hiyo ya kangamoko au 
baikoko ambayo watu wengi wameilalamikia
  kutokana na mtindo wanaoutumia,” alisema.Kundi la kangamoko limekuwa likilalamikiwa
mara kwa mara kutokana na kucheza wakionesha maungo ya miili yao wazi na kuvaa nguo nyepesi wanazozimwagia maji.Kukamatwa wasanii wa kundi hilo kumekuja siku chache tu tangu walalamikiwe katikaBunge la Jamhuri ya Muungano kwamba wamekuwawakipotosha jamnii.

comments

ALIYEMFUMANIA MKEWE GESTI AGEUZIWA KIBAO!

Baba Tony akiwa ametapakaa damu baada ya kufumaniwa akiwa na mke wa rafiki yake na kupewa kipigo.
 LILE sakata la hivi karibuni la mwanaume aliyefahamika kwa jina la Baba Asha kudai kumfumania mshikaji wake aitwaye Beda Mloka mkazi wa Ilala jijini Dar es Salaam akiwa na mkewe gesti,  limechukua sura mpya kufuatia aliyefumania kugeuziwa kibao na aliyedaiwa kufumaniwa.

Chanzo chetu cha kuaminika kilichoomba jina lake lisiandikwe juzi kililitonya  kuwa, mara baada ya fumanizi hilo lililotokea katika gesti iitwayo Pumzika iliyopo Msimbazi Center kisha aliyefumaniwa kuchezea kichapo, mambo yalikwenda chinichini lakini juzikati aliyefumania aliitwa Kituo cha Polisi, Pangani.
“Lile tukio lilikuwa gumzo sana pale mtaani kwetu, na kwa aibu Beda alitoweka kwa siku kadhaa lakini juzi Baba Asha akaitwa polisi, inavyoonekana mgoni kamgeuzia kibao mwenzake.
Mke wa Baba Asha akiwa amejiinamia baada ya songombingo kutokea.
“Nilijaribu kudadisi nikasikia Beda anadai Baba Asha na mkewe wamemchezea chezo na anajaribu kuonesha kuwa hakufumaniwa, kitu ambacho kinawashangaza wengi kutokana na mazingira waliyokutwa gesti,” alidai mtoa habari huyo.
Katika kujua ukweli wa sakata hili, mwandishi wetu alimtafuta Beda bila mafanikio lakini Baba Asha alipopatikana alisema: “Ni kweli leo (Jumatano ya juzi) niliitwa pale Polisi Pangani, jamaa niliyemfumania na mke wangu kaenda kunishitaki kuwa nimemfanyia mchezo.
“Kwa kweli ni jambo la kushangaza sana, yaani kanitibulia ndoa yangu halafu ananigeuzia kibao! Tutaona sasa yeye na mimi nani ataumbuka. Nimetakiwa kwenda kuripoti tena pale polisi kesho (jana) na baada ya hapo nitajua nini cha kufanya.”
KUSOMA HABARI YA SAKATA HILI >> BONYEZA HAPA<<
comments

DIAMOND ATOBOA KWANNINI AMEKUWA KIWEMBE KWA WANAWAKE

                                                                                                                                                                              KWA mara ya kwanza nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond' ameacha gumzo London, Uingereza baada ya kueleza sababu za kwa nini ni kiwembe?

Akifunguka katika mahojiano maalum wiki iliyopita na Kipindi cha Sporah Show cha runingani alipokuwa kwenye ziara ya kimuziki nchini humo, Diamond alizungumza ishu kibao za kimapenzi hasa juu ya msururu wa wanawake ambao tayari ametoka nao.
ASISITIZA ANASUBIRI MTOTO
Kabla ya yote, staa huyo alisisitiza kuwa muda si mrefu anatarajia kupata mtoto kutoka kwa mpenzi wake wa sasa, Peniel Mungilwa ‘Penny’ akimaanisha kuwa ni mjamzito, kinyume na msichana huyo ambaye hivi karibuni alimshangaa Diamond kueneza habari hizo.
KWA NINI ANAPENDA KUBADILISHA WANAWAKE?
Diamond: Mimi ni binadamu kama binadamu wengine wa kawaida. Nampenda mwanamke anayenipenda na kuniheshimu. Ikitokea mikwaruzano huwa mimi nakaa pembeni, natafuta sehemu nyingine. Wakati mwingine mimi ndiye huwa naachwa.
KWA NINI MSURURU NDANI YA KIPINDI CHA MIAKA MITATU?
Diamond: Nikiwa na mtu nikiachana naye naonekana nina matatizo kwa sababu wakati mwingine nakuwa na wanawake wenye majina. Siwezi kukaa bila uhusiano na nakuwa wazi kwa sababu lazima itajulikana tu na kuandikwa kwenye magazeti. Kuna kipindi nilikaa miezi sita bila kufanya kitu chochote (mh!). Lakini nikianza (uhusiano), nikihama naonekana msumbufu.
KWA NINI MASTAA, TENA MARAFIKI?
Diamond: Huwa sitoki, nakuwa nyumbani tu, nakaa na mama yangu (Sanura Kassim ‘Sandra’) nampikia. Nikitoka nakwenda kwenye shoo au studio. Huko ndiko nakutana nao (mastaa wa kike).
ALIMPATAJE JOKATE (MWEGELO)?
Diamond: Alikuwa anazindua nguo zake (Kidoti) akaniomba nikapite nazo kwenye onesho la mavazi, nikapita nazo jukwaani. Baada ya hapo na mimi nilimuomba nifanye naye video ya wimbo wangu (Mawazo), ndiyo ikatokea kama hivyo.
NINI KILIMVUTIA KWA PENNY?
Diamond: Kwanza mimi nilimjua Penny kabla ya Wema (Sepetu), alikuwa mshikaji wangu. Ni mwanamke mzuri, wa kileo, ana akili adabu na heshima. Anampenda mama yangu na familia yangu ‘coz’ na mimi nampenda mama yangu (sifa ambazo kwa mujibu wake Wema alizikosa).
KWA NINI ALIMREKODI WEMA?
Diamond: Kila binadamu anajiona yupo sawa na anaonewa. Sipendi kuongea, nitazungumza vibaya. Mapenzi yanaumiza na mimi naumia pia lakini watu wanadhani mimi ndiye muumizaji. Unamwambia mtu kwa nini una mwanaume mwingine.
Anakuzuga sijui ni pedeshee anampa pesa. Mara unamwona na mwanaume mwingine. Mimi siyo maskini lakini sasa mara unamwona na brazameni mwingine ‘then’ washkaji wanakwambia. Wewe unajifanya kuziba masikio mara unasikia ana mwanaume mwingine. Lakini ikafika wakati nikajikuta naumia sana kwenye mapenzi.
 
Kama ukisikiliza ule wimbo wa Kesho ni kweli kabisa. Mimi nikakaa pembeni hadi nilipompata huyu wa sasa (Penny).
Nakumbuka (Wema) alinipigia simu akadai mimi ndiye nasema anataka turudiane. Nilikuwa kwenye gari, nikamuuliza anataka nini?
Wakati huo nilishafika nyumbani kwa baby wangu. Nikamwonesha ona sasa, anasema mimi ndiyo nataka nirudiane naye, anatangazia watu hadi saluni kuwa nataka kurudiana naye na kujidai kwenye vyombo vya habari kuwa ananipenda. Kumbe ana wengine (ving’asti) kama ishirini anawahonga (mistari ya wimbo wake wa Nataka Kulewa).
 
Nilimpa baby wangu akamwambia kistaarabu tuache tulale. Sasa kuna mtu wetu wa karibu ndiye aliyehusika kusambaza ile sauti.
SEMA UKWELI, ULILALA NA UWOYA?


Diamond: (kicheko) Ningeanzia wapi? Unajua mimi ni simba kwa hiyo nikionekana na swala inajulikana lazima nimle hata kama tumeenda sehemu tu kuzungumza ishu za kazi.
KWA NINI WANAWAKE AU ENZI ZILE HAKUWA NA ‘CHANSI’ SASA AMEPATA?
Diamond: Ukimuelimisha mwanamke mmoja umeelimisha ulimwengu mzima. Nawapenda sana, wanajaa tele kwenye shoo zangu. Kilichotokea kwa Wema ilibidi tu sikuwa na jinsi.
ANATAKA MWANAMKE WA AINA GANI?
Diamond: Ukimuuliza mwanamke aliyewahi kuwa na mimi atakwambia najua mapenzi, najua kupetipeti, najua kubembeleza, najua kujifanya mjinga. Narudia tena, awe mzuri, wa kileo, mwenye akili, anayejiheshimu, ampende mama yangu kama mimi ninavyompenda mama yangu.
KWA NINI KIWEMBE?
Uchunguzi uliofanywa ulibaini kuwa chanzo cha staa huyo aliyetokea Tandale, Dar kuitwa kiwembe ni kutokana na tabia yake ya kubadilisha wanawake kama nguo.

Baadhi ya aliowahi kuripotiwa akidaiwa kutoka nao ni Rehema Fabian (Miss Kiswahili 2009), Jacqueline Wolper (msanii wa filamu), Upendo Moshi ‘Pendo’ (Mshiriki wa Maisha Plus) na  Natasha (Video Queen wa Bongo Fleva).
 
Wengine ni Wema (mwigizaji), Jokate (mwigizaji), Aunt Ezekiel (mwigizaji), Najma (msanii wa Bongo Fleva), Penny (mtangazaji DTV), Irene Uwoya (mwigizaji) na wengineo.




KUNGALIA VIDEO YA MAHOJIAONO >>BOFYA HAPA<<
comments
...hii ni mtaa hadi mtaa...

VITUKO VYA MTAA Copyright © 2011 -- Template created by